Date:
29-10-2021
Reading:
Mithali 10:27-30
Ijumaa asubuhi 29.10.2021
Mithali 10:27-30
[27]Kumcha BWANA kwaongeza siku za mtu; Bali miaka yao wasio haki itapunguzwa.
[28]Matumaini yao wenye haki yatakuwa furaha; Bali kutaraji kwao wasio haki kutapotea.
[29]Njia ya BWANA ni kimbilio lake mtu mkamilifu; Bali ni uharibifu kwao watendao maovu.
[30]Mwenye haki hataondolewa milele; Bali wasio haki hawatakaa katika nchi.
Tukaze mwendo katika Yesu Kristo;
Suleiman anaonesha kuwa kumcha Bwana huongeza siku zake aaminiye. Kumcha Bwana huleta tumaini, na kimbilio kwa wakamilifu. Wenye haki hustarehe milele, bali wasio haki mwisho wake ni kuangamia.
Suleiman anatukumbusha kuishi maisha ya kumcha BWANA ili kuwa na mwisho mwema. Hatma yetu itategemea tulivyoishi katika njia yetu ya ufuasi. Fanya uchaguzi bora wa kumcha Bwana ili usiondolewe milele, bali furaha yake iwe kwako milele.
Siku njema.