Date: 
20-06-2018
Reading: 
Phillipians 2:12 (Wafilipi 2:12)

WEDNESDAY 20th June 2018
“...Work out your own salvation with fear and trembling” (Phil. 2:12)

Holy fear must never disappear from the heart of a Christian. When fear is no longer present, the soul is on its deathbed. Just consider what is at stake for you;
Eternity in Heaven or Hell,
Salvation or Damnation
An Almighty and Holy God, or A powerful adversary of the soul, Satan
And you think a puny child of man should not tremble when he considers these alternatives?
But one should not worry, because one would always experience a secret trembling within the heart. This is not a mark of death, but of life. It is this trembling which keeps one’s assurance of salvation from becoming carnal security.
If, however, this holy fear is at the point of death, then wake up in earnest! It may soon be too late. Heaven is not reached by a path of ease. Fear is always - to keep you awake and drive you to your God, whom you not only fear, but love.
Work out your own salvation in fear and trembling.

 



JUMATANO TAREHE 20 JUNI 2018
“..utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.” (Flp 2:2)

Hofu ya Mungu haitakiwi kuondoka katika nafsi ya Mkristo yeyote! Kwa kuwa hofu ya Mungu ikiondoka, nafsi huwa imekufa. Hebu tafakari UCHAGUZI huu ufuatao ukiwa mbele yako ili uchague:
Mbinguni au Jehanum;
Kuokolewa au Kuangamia milele.
Kuwa na Mungu, au kuwa na adui Shetani
Ni nani baada ya kuyatafakari haya asipate chembe ya moyo ya woga? Lakini hata kama unapatikana woga, Usiogope mtu wa Mungu, woga huo si dalili ya kifo bali ni dalili kwamba kuna uzima nafsini kwako! Ni woga huu ndio unaotukumbusha na kutupa tumaini la wokovu na kuepuka kuwa wahudumu wa dunia hii. Lakini pale woga huu utakapoashiria kifo cha imani, basi zinduka mwenzangu, kwani mwisho wako unakunyemelea kwa kasi, na utakujia ghafula na kukupoteza. Kunga mambo ya mbinguni kunahitaji juhudi. Hofu ya Mungu ina lengo la kukuamsha na kukumbusha kujipanga kwa upya kulitimiza kusudi la Mungu, umche na kumpenda!
Ndiyo maana tunakumbushwa tuutimize wokovu wetu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka!