Date: 
12-02-2020
Reading: 
Matthew 20:1-16

WEDNESDAY 12TH FEBRUARY 2020 MORNING                                   

Matthew 20:1-16 New International Version (NIV)

1“For the kingdom of heaven is like a landowner who went out early in the morning to hire workers for his vineyard. He agreed to pay them a denarius[a] for the day and sent them into his vineyard.

“About nine in the morning he went out and saw others standing in the marketplace doing nothing. He told them, ‘You also go and work in my vineyard, and I will pay you whatever is right.’ So they went.

“He went out again about noon and about three in the afternoon and did the same thing. About five in the afternoon he went out and found still others standing around. He asked them, ‘Why have you been standing here all day long doing nothing?’

“‘Because no one has hired us,’ they answered.

“He said to them, ‘You also go and work in my vineyard.’

“When evening came, the owner of the vineyard said to his foreman, ‘Call the workers and pay them their wages, beginning with the last ones hired and going on to the first.’

“The workers who were hired about five in the afternoon came and each received a denarius. 10 So when those came who were hired first, they expected to receive more. But each one of them also received a denarius. 11 When they received it, they began to grumble against the landowner. 12 ‘These who were hired last worked only one hour,’ they said, ‘and you have made them equal to us who have borne the burden of the work and the heat of the day.’

13 “But he answered one of them, ‘I am not being unfair to you, friend. Didn’t you agree to work for a denarius? 14 Take your pay and go. I want to give the one who was hired last the same as I gave you. 15 Don’t I have the right to do what I want with my own money? Or are you envious because I am generous?’

16 “So the last will be first, and the first will be last.”

Jesus has made us equal, so we need to be careful that we do not judge others by using our own standards. Jesus selects and calls his workers from among those who appear foolish, and from among the weak and the humble.


JUMATANO TAREHE 12 FEBRUARI 2020  ASUBUHI                       

MATHAYO 20:1-16

1 Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu.
Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu.
Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi;
na hao nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda.
Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile.
Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?
Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, enendeni nanyi katika shamba la mizabibu.
Kulipokuchwa, yule bwana wa shamba akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ujira wao, ukianzia wa mwisho hata wa kwanza.
Na walipokuja wale wa saa kumi na moja, walipokea kila mtu dinari.
10 Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba watapokea zaidi; na hao pia wakapokea kila mtu dinari.
11 Basi wakiisha kuipokea, wakamnung'unikia mwenye nyumba,
12 wakisema, Hao wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana kutwa.
13 Naye akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari?
14 Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe.
15 Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema?
16 Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho.

Yesu ametuweka wote kuwa sawa mbele zake, hivyo tunahitaji kuwa makini ili tusije tukawahukumu wengine kwa kutumia vigezo vyetu wenyewe. Yesu anachagua na kuwaita wafuasi wake miongoni mwao wanaoonekana kuwa wajinga, na kati ya walio dhaifu na wanyenyekevu.