Date: 
03-03-2022
Reading: 
Mathayo 9:9-13

Hii ni Kwaresma 

Alhamisi asubuhi tarehe 03.03.2022

Mathayo 9:9-13

9 Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona mtu ameketi forodhani, aitwaye Mathayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata.

10 Ikawa alipoketi nyumbani ale chakula, tazama, watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuja wakaketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake.

11 Mafarisayo walipoona, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?

12 Naye aliposikia, aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi.

13 Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.

Kutubu na kurejea kwa Bwana;

Mafarisayo na watoza ushuru hawakubaliani suala la Yesu kukaa na kula na wenye dhambi. Lakini Yesu anawasikia na kuwaelimisha, kuwa amekuja kwa ajili ya watu wake wote. 

Yesu anatukumbusha kuwa alikuja kwa ajili yetu sote, wala habagui kama ambavyo wapo baadhi yetu ambao hujiona ufalme wa Mungu ni wao peke yao. Huwaona wengine hawafai kumwendea Yesu! Yesu anatuita kutubu na kumrejea ili tuwe na hatma njema. 

Uwe na siku njema.