MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 13 AGOSTI, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI MWENENDO WENU UWE NA HEKIMA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni:  Hakuna wageni waliotufikia na cheti:

3. Uongozi wa Kanisa Kuu Azania Front,  pamoja na Kamati ya Misioni na Uinjilisti ya Baraza la Wazee, inamshukuru Mungu kwa kukamilisha semina ya siku 9 iliyoanza Alhamisi tarehe 03 Agosti hadi Ijumaa tarehe 11 Agosti kwa ushindi mkubwa.  Hakika tulimuona Mungu akifanya mabadiliko makubwa kwa watu mmoja mmoja na mazingira.   Mnenaji katika Semina hiyo alikuwa ni Mwl. Grace Kisuu, ambaye sasa anaelekea Tanga kwa huduma.  Kwa ajili huduma iliyofanyika hapa, leo tutaendelea na maombi hapa Usharikani.  Tutakuwa na kipindi cha kufundishwa maana, kusudi na jinsi ya kuomba, mwalimu atakuwa Mch. David Nkone.  Na baadaye tutakuwa na zoezi la kuomba tukiongozwa na Mtumishi Mcharo aliye katika huduma ya mwalimu Grace Kisuu.  Huduma hii inafanyika ndani ya Kanisa hapa Usharikani kuanzia saa kumi kamili jioni.  Karibuni wote na hakuna kiingilio.

4. Tunapenda kusisitiza tena kwa washarika, kwamba wale wanaodaiwa madeni ya mavuno ya Mwaka jana 2016 na miaka ya nyuma warejeshe madeni yao ofisi ya wahasibu.

5. Washarika wote kwa kuheshimu utakatifu na uchaji ibadani  mnakumbushwa kuvaa mavazi yenye staha na yanayompa Mungu heshima na utukufu ibadani.  Hili tunalikumbusha tukijua kuwa washarika wa Kanisa Kuu na wageni wao na familia zao ni waelewa na wachaji wa ibada.

6. Leo Mchungaji Chuwa yupo Mtaa wa Kiharaka kwa huduma za kichungaji akiongozana na Kwaya ya Tarumbeta.

7. Vitenge vya Kiharaka bado vipo, vitauzwa hapo nje kwa bei ya shilingi elfu 10.  Kama umeshanunua unaweza kumnunulia ndugu, rafiki ili tuweze kufanikisha ujenzi wa kituo chetu cha Kiroho Kiharaka.  

8. Jumanne ijayo tarehe 15/08/2017 saa 11.00 jioni. Kutakuwa na maombi ya pamoja kwa Viongozi wa mitaa yote ya Nyumba kwa Nyumba yatakayofanyika  hapa Usharikani.  

9. Mkutano wa VICOBA ya  Wajane na Wagane wa Azania Front utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 26 Agosti, 2017 kuanzia saa 3.00 asubuhi.  Wahusika wote wanaombwa kuhudhuria.

10. Usharika kupitia Kamati ya Uhusiano na Habari, una mkakati wa kuwahabarisha Washarika kwa kijarida kitakachokua na habari mbali mbali za Usharika, vikundi na mitaa yake.  Kijarida hicho kitatoka kila baada ya miezi 3.  Kamati inatafuta mtu mwenye taaluma husika kufanya kazi hiyo, kwa ujira na maelewano maalum.  Kwa mawasiliano zaidi muone Mzee T. Mlaki, Mzee C. Swai au katibu wa Usharika.

11. Uongozi wa Umoja wa Wanawake, unapenda kuwashukuru wanawake wote waliohudhuria Semina jana jumamosi tarehe 12.08.2017 iliyofanyika Usharika wa Kinyerezi.  Mungu awabariki sana.

 

12.  NDOA

NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 26/08/2017

SAA 10.00 JIONI

Bw. Winston Churchil katwaza        na     Bi. Lucy Zebedayo Lushiku

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 19/08/2017

SAA 8.00 MCHANA

Bw. Jackson Daudi Mukangara       na     Bi. Shirley Aggrey Mlimuka

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. Mugisha Kassano Mboneko      na     Bi. Evangelina Ephraim

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

13. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi S.H. Mbwilo
  • Kinondoni: Kwa Prof. G. Mmari
  • Ilala ¦ Chang’ombe ¦ Mivinjeni: Bwana na Bibi Kowero
  • Kawe ¦ Mikocheni ¦ Mbezi Beach: Kwa Prof. Esther Mwaikambo
  • Oysterbay ¦ Masaki: Kwa Bwana na Bibi Witson Moshi
  • Tabata: Watatangaziana
  • Kijitonyama ¦ Sinza ¦ Mwenge ¦ Makumbusho ¦ Ubungo: Kwa Bwana na Bibi C. Lyimo
  • Mjini kati: Kwa Bwana na Bibi G. Mnyitafu
  • Wazo ¦ tegeta ¦ Kunduchi ¦ BahariBeach ¦ Ununio:Kwa Bwana na Bibi Allen David

14. Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Kwanza

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.