Date: 
11-06-2017
Reading: 
Marko 2:1-5 {Mark 2:1-5}

ROHO MTAKATIFU NDIYE MSAADA WETU: UNA SHAUKU KIASI GANI?

Marko 2:1-5

1 Akaingia Kapernaumu tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani. 
2 Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake. 
3 Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne. 
4 Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza. 
5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.

Mungu anapoiona imani ilivyojaa shauku ya kupata toka kwake kile alichomwandali mtu wake, hataidharau kamwe, bali ataishangilia. Tukisoma Mathayo 11:12 neno linasema;

   " Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka" 

Kama ndani kwako hakuna shauku, hakuna msukumo, jua kuwa utasubiri muda mrefu kupata haja ya moyo wako, wako ambao kwa shauku waliyonayo watakupita, wapate wao kwanza. Na kama una nguvu kiasi, basi utasogea mbele kidogo, japo upate kidogo. Lakini kama una shauku ya kweli, na ukitaka kwa moyo utapewa kipaumbele katika kupokea haja ya moyo wako, bila kujali wengine wamesubiri kwa muda gani. Watu wenye shauku ni ving'ang'anizi, hawaachilii mpaka jibu litoke.  Na katika kutafuta kila mtu atajua kuwa huyo ana mahitaji. Ingawa  watu ving'ang'anizi wanasumbua, hawajali wanamsumbua nani, ili mradi wapate wanachokitaka. Wewe una shauku kiasi gani cha kutaka Mungu aingilie kati mambo yako? Mwite Mungu leo, asikie hamu na shauku  uliyo nayo juu yake ndani ya sauti yako na vitendo vyako, hakika atakujibu mara. Alimtuma Roho wake kwetu kwa kusudi hilo, ili furaha yetu itimilike.

HOLY SPIRIT IS OUR HELPER: HOW DESPERATE ARE YOU?

Mark 2:1-5

Jesus Forgives and Heals a Paralyzed Man

1 A few days later, when Jesus again entered Capernaum, the people heard that he had come home. They gathered in such large numbers that there was no room left, not even outside the door, and he preached the word to them.Some men came, bringing to him a paralyzed man, carried by four of them. Since they could not get him to Jesus because of the crowd, they made an opening in the roof above Jesus by digging through it and then lowered the mat the man was lying on. When Jesus saw their faith, he said to the paralyzed man, “Son, your sins are forgiven.”

When God sees desperate faith in action, He is most unlikely to turn it down. In fact, God allows such. Reading from Mathew 11:12, the Word says;

    " And from the days of John the Baptist until now the kingdom of heaven suffers violence, and the violent take it by force!"

If you are not desperate, you would be placed at the end of the line. If you are a bit violent, you can end up in the middle of the queue, but if you are truly desperate, you will be moved to the front, irrespective of how long others have waited to get there. 

Desperate people are persistent. They draw up attention of other people in their bid to get what they desire. Although desperate people can really be a "nuisance", they do not care about who they convenience as long as they get what they get what they want. 

How desperate are you for divine intervention over your situation? Cry out to God today and let Him hear the desperation in your voice and see it in your action, and He will surely answer you. He sent His Holy Spirit to us just for that, so that our joy be complete.