MATANGAZO YA USHARIKA 

TAREHE 03 MACHI, 2024

SIKU YA BWANA YA 4 KABLA YA PASAKA

NENO LINALOTUONGOZA NI

TUMTAZAME BWANA ALIYE TUMAINI LETU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 25/02/2024

4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. 

6. Jumatano ijayo tarehe 6/03/2024 saa 11.00 jioni tutaendelea na ibada ambayo itaongozwa na Wanawake kurudia maombi ya dunia. Na Jumapili ijayo tarehe 10/03/2024 wanawake wataongoza ibada zote.

7. Leo tarehe 03/03/2024 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika Karibuni.

8. MAFUNDISHO KATIKA KIPINDI CHA KWARESMA 2024 yanaendelea kila siku ya kila Ahamisi na Ijumaa, kuanzia saa 11:00 jioni, kila siku, waalimu mbalimbali watafundisha. Katika vipindi hivyo tutakuwa na Mafundisho, Maombi na Maombezi. Kichwa cha mafundisho hayo ni 

" NIA YA UPENDO WA KRISTO KWA FAMILIA " Neno la kusimamia ni kutoka Yoe‬l 2:12-‬14‬ ‬‬‬‬‬‬‬‬ Wote mnakaribishwa."‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬‬

9. Jumamosi ya tarehe 23/03/2024 kutakuwa na Ibada ya Wazee kuanzia miaka 60 na kuendelea. Ibada itafanyika hapa usharikani Azania Front Cathedral kuanzia saa 3.00 asubuhi ambayo itaambatana na Chakula cha Bwana. Mungu awabariki.

10. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: Kwa Mama Violet Maro
  • Mjini kati: Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Watatangaziana
  • Kinondoni: Kwa Prof. Geofrey Mmari
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Adv. Joseph na Adv. Vupe Mpuya
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Oysterbay, Masaki: Watashiriki ibada za jumatano hapa Kanisani

11. Zamu za wazee ni kundi la Kwanza.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.