Date: 
07-03-2018
Reading: 
Acts 2:22-28 (Matendo 2:22-28)

WEDNESDAY 7TH MARCH 2018 MORNING                      

Acts 2:22-28 New International Version (NIV)

22 “Fellow Israelites, listen to this: Jesus of Nazareth was a man accredited by God to you by miracles, wonders and signs, which God did among you through him, as you yourselves know. 23 This man was handed over to you by God’s deliberate plan and foreknowledge; and you, with the help of wicked men,[a] put him to death by nailing him to the cross. 24 But God raised him from the dead, freeing him from the agony of death, because it was impossible for death to keep its hold on him. 25 David said about him:

“‘I saw the Lord always before me.
    Because he is at my right hand,
    I will not be shaken.
26 Therefore my heart is glad and my tongue rejoices;
    my body also will rest in hope,
27 because you will not abandon me to the realm of the dead,
    you will not let your holy one see decay.
28 You have made known to me the paths of life;
    you will fill me with joy in your presence.’[b]

Footnotes:

  1. Acts 2:23 Or of those not having the law (that is, Gentiles)
  2. Acts 2:28 Psalm 16:8-11 (see Septuagint)

The above is part of a sermon by The Apostle Peter on the day of Pentecost. It includes a quotation from the Book of Psalms.  Peter preached a powerful sermon about the coming of the Holy Spirit and the work of Jesus Christ.

3000 people believed and were baptized that day which we regard as the official start of the Christian Church.

Thank God that the Gospel is still preached today and people are coming to faith all over the world. Pray that many more would come to faith and the Church would continue to grow in numbers and spirituality.

JUMATANO TAREHE 7 MACHI 2018 ASUBUHI                        

MATENDO 2:22-28

22 Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua; 
23 mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua; 
24 ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao. 
25 Maana Daudi ataja habari zake, Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko upande wa mkono wangu wa kuume, nisitikisike. 
26 Kwa hiyo moyo wangu ukapendezewa, ulimi wangu ukafurahi; Tena mwili wangu nao utakaa katika matumaini. 
27 Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu; Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu. 
28 Umenijuvisha njia za uzima; Utanijaza furaha kwa uso wako. 
 

Maneno haya juu ni sehemu ya mahubiri ya Mtume Petro siku ya Pentekoste. Pia alinukuu sehemu ya Kitabu cha Zaburi.

Siku ile Mungu alituma Roho Mtakatifu. Petro alifundisha kuhusu Roho Mtakatifu na kazi za Yesu Kristo. Watu 3000  waliamini Injili na kubatizwa siku ile. Tunahesabu kama siku ya kuzaliwa kwa Kanisa la Kristo.

Tumshukuru Mungu kwamba Injili inaendelea kuhubiriwa na watu wanaokoka duniani kote. Omba kazi hii iendelee vizuri na kanisa likuwe kiidadi na Kiroho.