Date: 
05-11-2018
Reading: 
1 Thessalonians 3:11-13

MONDAY 5TH NOVEMBER 2018 MORNING                     

1 Thessalonians 3:11-13 New International Version (NIV)

11 Now may our God and Father himself and our Lord Jesus clear the way for us to come to you. 12 May the Lord make your love increase and overflow for each other and for everyone else, just as ours does for you.13 May he strengthen your hearts so that you will be blameless and holy in the presence of our God and Father when our Lord Jesus comes with all his holy ones.

The Apostle Paul wrote these words of encouragement to the Christians at Thessalonica.  He prayed for them that they might grow spiritually. He wants them to be Holy.

It is God’s desire for all Christians to be sanctified as we are guided by the Holy Spirit and produce the fruit of the Spirit.

This doesn’t happen automatically. We need to keep rejecting sin and choosing what is right. We need to spend time in Bible reading and prayer and Christian Fellowship.

JUMATATU  TAREHE 5 NOVEMBA 2018 ASUBUHI                 

1 THESALONIKE 3:11-13

11 Basi Mungu mwenyewe, Baba yetu, na Bwana wetu Yesu, atuongoze njia yetu tufike kwenu. 
12 Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu; 
13 apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.

Mtume Paulo aliandika maneno haya kuwatia moyo Wakristo kule Thesalonike. Alitamani wote wakue kiroho na kutakaswa. Mungu anataka sisi sote tuwe watakatifu. Utakaso unapaswa kuwa endelevu. Hautokei hivihivi tu. Itabidi tujitahidi kukataa dhambi na kuchagua yalio mema kila wakati. Tutii mwongozo wa Roho Mtakatifu ili tuweze kuzaa Matunda ya kiroho. Pia tuwe na bidii katika maombi na kusoma Neno la Mungu, na kufika ibadani kanisani na za Nyumba kwa nyumba, kujumuika na Wakristo wenzetu na kutiana moyo.