Date: 
23-03-2023
Reading: 
Yohana 6:51

Hii ni Kwaresma 

Alhamisi asubuhi tarehe 23.03.2023

Yohana 6:51

Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.

Yesu ni chakula cha uzima;

Sura ya sita ya Injili ya Yohana inaanza kwa kusimulia juu ya ishara ya kulisha watu elfu tano kwa mikate mitano na samaki wawili. Na baada ya ishara hiyo ndipo Yohana anaandika Yesu akijitambulisha kama chakula cha uzima. Ni ujumbe ambao ulizua taharuki, maana wayahudi hawakumwelewa! Walifikiri aliwaambia wale mwili wake kama walivyomuona.

Yesu aliposema yeye ni chakula cha uzima, alimaanisha yeye ndiye aliyetoka mbinguni kuuokoa ulimwengu. Watu waliamini katika chakula ili waendelee kuwepo, lakini Yesu alitoka mbinguni kama chakula chenye uzima ili ulimwengu wote uokolewe katika yeye. Mwamini yeye uokolewe 

Alhamisi njema.

 

Heri Buberwa 

Mlutheri