Date:
01-11-2024
Reading:
1Wakorintho 1:18-19
Ijumaa asubuhi tarehe 01.11.2024
1 Wakorintho 1:18-19
18 Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.
19 Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili nitazikataa.
Mwenye haki ataishi kwa imani;
Mtume Paulo anawaonesha watu wa Korintho nguvu ya msalaba katika kuwaokoa wanadamu. Anasema msalaba ni nguvu ya Mungu kwetu tunaookolewa, bali kwao wanaopotea ni upuuzi. Kwa mujibu wa Mtume Paulo, hekima na akili ya kweli ni kumwamini Kristo aliyekufa msalabani.
Msalaba ni nguvu ya Mungu kwa sababu Yesu alikufa msalabani sisi tukaokolewa. Tofauti yetu na wasioamini ni kwamba sisi tunayo neema ya msalaba. Ni neema kwa sababu ya wokovu tuliopewa bure kwa njia ya kifo cha Yesu msalabani. Jambo la muhimu ni kutomuacha Yesu aliyekufa msalabani kwa ajili yetu. Ubarikiwe
Heri Buberwa