Date:
05-08-2024
Reading:
Mithali 19:8
Jumatatu asubuhi tarehe 05.08.2024
Mithali 19:8
Apataye hekima hujipenda nafsi yake; Ashikaye ufahamu atapata mema.
Sura ya 19 ya Mithali inaandika juu ya kuenenda katika Bwana. Ni Mithali juu ya kumcha Bwana, kuacha upumbavu na kuenenda kwa maarifa. Mstari wa kwanza kabisa unaeleza juu ya kuenenda katika Bwana;
Mithali 19:1
Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake, Kuliko mpotofu wa midomo aliye mpumbavu.Mstari tuliosoma unakazia hekima ili kujipenda nafsi, yaani hekima kumuongoza aaminiye kuiokoa nafsi kwa kumwamini Yesu.
Ujumbe mkuu wiki hii ni kuenenda kwa hekima. Kama somo linavyosema, hekima ni njema maana hutuokoa nafsi. Kwa hekima tunakuwa na ufahamu ambao hutupeleka kwa Yesu. Tuombe neema ya Mungu atujalie hekima ili tupate kutenda kwa usahihi katika njia ya ufuasi.
Tunakutakia wiki njema yenye kuenenda kwa hekima. Amina.
Utume mwema
Heri Buberwa