Date:
02-07-2024
Reading:
Mathayo 12:46-50
Jumanne asubuhi tarehe 02.07.2024
Mathayo 12:46-50
46 Alipokuwa katika kusema na makutano, tazama, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wataka kusema naye.
47 Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe.
48 Akajibu, akamwambia yule aliyempasha habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani?
49 Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu!
50 Kwa maana ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.
Ninyi ni barua ya Kristo;
Yesu alikuwa amekwenda Yerusalemu na wazazi wake. Wakati wa kurudi nyumbani wakagundua kwamba hawakuwa na Yesu kwa maana ya kuwa alibaki Yerusalemu. Ndipo tunaona Yesu akiambiwa kwamba ndugu zake wako nje wanataka kusema naye. Alitoa jibu ambalo wengi hawakulitegemea, kwanza anauliza mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni nani? Akasema wafanyao mapenzi ya Mungu ndiyo ndugu zangu.
Yesu hakuwakataa ndugu zake, bali ilikuwa katika kuendelea kufundisha na kuonyesha kuwa yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Alijua, kuwa tayari watu walijua kuwa walioko nje ni ndugu zake. Lakini kama Mungu Mwokozi, alikuwa akiwataka wasikilizaji wake kufanya mapenzi ya Mungu kama alivyofundisha. Aliwataka kuwa barua inayosomeka vizuri. Nasi tunakumbushwa kuwa barua inayosokeka vizuri. Amina
Jumanne njema.
Heri Buberwa