Date:
20-06-2024
Reading:
Warumi 10:14-15
Alhamisi asubuhi tarehe 20.06.2024
Warumi 10:14-15
14 Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?
15 Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!
Umoja wetu, nguvu yetu;
Mtume Paulo anatamani watu wote waokolewe kwa Injili anayoihubiri. Ni kwa sababu injili ni kwa ajili ya watu wote, maana baada ya Yesu Kristo hakuna Myahudi wala Myunani. Kwa hiyo Yesu lazima ahubiriwe kwa watu wote. Ndiyo maana Paulo anauliza; wamwiteje yeye wasiyemwamini? Wamwaminije wasipomsikia? Na wamsikieje pasipo mhubiri?
Kumbe Paulo hapa anatukumbusha kuhubiri Injili ili watu wote waokolewe. Katika hili Paulo anauliza; wahubirije wasipopelekwa? Hapa upo ujumbe kwamba lazima tutoe vipawa vyetu kwa ajili ya Injili. Hapa mtu mmoja hawezi, bali kila mmoja kutoa kwa kadri ya alivyojaliwa ili kuitenda kazi ya Mungu. Ndiyo maana umoja wetu ni nguvu yetu. Amina.
Alhamisi njema.
Heri Buberwa