Date: 
05-07-2022
Reading: 
Mwanzo 39:6-12

Jumanne asubuhi tarehe 05.07.2022

Mwanzo 39:6-12

6 Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu cho chote chake, ila hicho chakula alichokula tu.

7 Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami.

8 Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu.

9 Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?

10 Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye.

11 Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani;

12 huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje.

Kijana na uchumi katika zama za utandawazi;

Potifa alikuwa akida wa Farao, akiwa mkuu wa askari katika Misri. Ndiye aliyemnunua Yusufu kutoka kwa Waishmaeli, akamweka nyumbani mwake kama mtumishi. Habari tunayosoma asubuhi hii ni Yusufu akilazimishwa kulala na mke wa Potifa, lakini anakimbia na kuacha nguo yake mikononi mwa mke wa Potifa!

Hii ikitokea leo ni fursa kwa baadhi ya vijana! Kwamba anaitwa na mwanamke alale naye?! Ni fursa! 

Ila mimi nakwambia, siyo fursa, ni dhambi. Yusufu aliikimbia dhambi kwa mguu. Dhambi inakimbiwa hata kwa mguu. Ikimbie dhambi ili Bwana akurehemu.

Siku njema.