Date: 
15-09-2022
Reading: 
Mithali 3:27-28

Alhamisi asubuhi tarehe 15.09.2022

Mithali 3:27-28

[27]Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, 

Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda.

[28]Usimwambie jirani yako, 

Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa; 

Nawe unacho kitu kile karibu nawe.

Jirani yako ni nani?

Zipo haki ambazo mtu anazo, bila kusubiri sheria. Hizi zipo kwa mtu yeyote, maadamu anaishi. Mfano ni haki ya kupata chakula na malazi. Haki nyingine pia zipo, lakini wakati mwingine hutegemea na sheria pia. Somo linasema usimnyime haki anayestahili, kama una mamlaka. Pia somo linakataza kumwambia mtu aje kesho wakati unaweza kumsaidia leo. Ukimcheleweshea mtu haki yake ni sawa na kumnyima.

Tunakumbushwa siyo kutenda haki tu, bali kutenda haki kwa wakati. Usipompa mtu haki kwa wakati unamuumiza, maana kuna kitu anakikosa, na pia anaweza asifikie malengo yake. Huu ni ukatili.

Acha kuwanyima watu haki zao kwa sababu tu ya mamlaka uliyo nayo. Utawajibika mbele za Mungu maana huo siyo ujirani tuliofundishwa na Yesu Kristo. Jirani yako ni nani?

Siku njema