MATANGAZO YA USHARIKA

                                   TAREHE 26 MACHI, 2023                       

                                  NENO LINALOTUONGOZA NI

                                       YESU NI MPATANISHI                             

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti.  

3. Matoleo ya Tarehe 19/03/2023

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wakumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

      NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

  • 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
  • Namba ya Wakala M-PESA 5795794KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa  Uongozi wa Mungu, Ibada za  mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu.  Alhamisi jioni saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

5. Ratiba yetu ya mafundisho katika msimu wa Kwaresma hapa Kanisa Kuu, inaendelea.

     a. Ibada ya Majivu siku ya Jumatano.  Kwaya zote zitahudumu. Zamu za  wazee itakuwa ni kundi l        la pili.

      b. Semina ya Neno la Mungu tarehe 29 hadi Ijumaa tarehe 31 Machi 2023. Vipindi vyote         vinaanza saa 11:00 jioni. Karibuni wote tumfanyie Mungu Ibada njema.

6. Jumamosi ijayo tarehe 01/04/2023 saa 3.00 asubuhi kutakuwa na ibada ya wazee kuanzia miaka 60.

7. Uongozi wa Wajane na Wagane unapenda kushukuru Uongozi wa Usharika kwa kufanikisha Semina yao nzuri iliyofanyika jana jumamosi tarehe 25/03/2023 saa 3.00 asubuhi mpaka saa 7.00 mchana hapa usharikani Azania Front  Cathedral. Mungu awabariki

8. Leo tarehe 26/03/2023 tutashiriki Chakula cha Bwana.  Washarika karibuni.

9. Uongozi wa Umoja wa Vijana Azania Front unapenda kuwaalika vijana wote kwenye mkesha utakaofanyikia hapa usharika Azania siku ya Ijumaa ya Tarehe 31/03/2023 kuanzia saa 3.00 usiku. Washarika wote mnakaribishwa.

10. SHUKRANI – JUMAPILI IJAYO TAREHE 02/04/2023 – KATIKA IBADA YA KWANZA       SAA 1.00 ASUBUHI

  • Familia ya Brighter Shirima watamshukuru Mungu kwa mambo mengi anayowatendea ikiwa ni pamoja na afya njema, ufaulu mzuri watoto wake katika mitihani yao ya kidato cha nne.

Neno: 1Wathesalonike 5:16-18, Wimbo: TMW 262

11. Jumamosi ijayo tarehe 01/04/2022 saa 2.00 asubuhi kutakuwa na maadhimisho ya pasaka Wanawake wote ngazi ya Jimbo yatakayofanyika Usharika wa Kipawa.  Wanawake wote mnaombwa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya maadhimisho hayo.

12. Kwaya ya Umoja itakuwa na mazoezi ya uimbaji siku ya Jumatatu saa 11.00 jioni kwa ajili ya maandalizi ya Ijumaa Kuu. Wanakwaya wote mnaombwa kuhudhuria na kwa wakati.

13. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Oysterbay na Masaki:/ Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach Watashiriki ibada hapa Usharikani
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: 
    • Kwa Mama Ruth Korosso
  • Mjini kati: …………………………
  • Ilala, Chang’ombe na Buguruni: ………………………..
  • Kinondoni: ……………………………………
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa …………..
  • Upanga: ……………………………………………                      
  • Tabata: Kwa Mch. Aston Kibona

14. Zamu: Zamu za wazee ni la Pili

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu,  Bwana ayabariki.