Date:
29-03-2023
Reading:
Luka 23:8-12
Hii ni Kwaresma
Jumatano asubuhi tarehe 29.03.2023
Luka 23:8.-12
8 Na Herode alipomwona Yesu alifurahi sana, kwa sababu alikuwa akitaka sana kumwona tangu siku nyingi, maana amesikia habari zake, akataraji kuona ishara iliyofanywa na yeye.
9 Akamwuliza maneno mengi, yeye asimjibu lo lote.
10 Wakuu wa makuhani na waandishi wakasimama wakamshitaki kwa nguvu sana.
11 Basi Herode akamfanya duni, pamoja na askari zake, akamdhihaki, na kumvika mavazi mazuri; kisha akamrudisha kwa Pilato.
12 Basi siku ile ile Herode na Pilato walipatana kwa urafiki kwa maana hapo kwanza walikuwa na uadui wao kwa wao.
Yesu ni mpatanishi.
Injili
ya Luka leo inatuonesha jinsi Yesu alivyoiendea njia ya mateso baada ya kukamatwa. Alipelekwa kwa Pilato, akahamishiwa kwa Herode, akarudishwa tena kwa Pilato. Pilato akazidiwa na nguvu ya umma iliyomlazimisha kummwachia Baraba na kumsulibisha Yesu.
Ni njia ya mateso katika kuukomboa Ulimwengu ambapo Yesu alifanyika sadaka ya upatanisho kati yetu na Mungu. Yesu alipotupatanisha na Mungu alituokoa na kutuleta kwa Baba ambako kuna uzima wa milele. Tukae na Yesu siku zote aliye Bwana na Mwokozi wetu. Amina.
Heri Buberwa