Date:
22-12-2021
Reading:
Luka 21:29-32
Hii ni Advent
Jumatano asubuhi tarehe 22.12.2021
Luka 21:29-32
29 Akawaambia mfano; Utazameni mtini na miti mingine yote. 30 Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu. 31 Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu. 32 Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie.
Bwana yu Karibu;
Yesu anaonesha ambavyo watu waliona mtini umechipuka na kungojea mavuno. Alitumia mfano wa mtini ambao ulikuwa katika mazingira husika. Ni kama sisi tunapoona mazao yetu yameota, mvua zikinyesha vizuri huwa tunajua mavuno yamekaribia, tukingojea mavuno kwa hamu.
Yesu alitumia mfano huu kuelezea ufalme wake, kuwa ukaribu. Kuwepo kwake naweza kusema ni mazao yanaendelea vizuri shambani. Mavuno yako karibu, yaani Yesu yu karibu kurudi.
Umejiandaaje ili anaporudi asikuache?
Uwe na Jumatano njema.