Jumatatu asubuhi tarehe 04.07.2022
Isaya 48:14-19
14 Kusanyikeni, ninyi nyote, mkasikie; ni nani miongoni mwao aliyehubiri haya? Bwana amempenda; atatimiza mapenzi yake juu ya Babeli, na mkono wake utakuwa juu ya Wakaldayo.
15 Mimi, naam, mimi, nimenena; naam, nimemwita; nimemleta, naye ataifanikisha njia yake.
16 Nikaribieni, sikieni haya; tokea mwanzo sikunena kwa siri; tangu yalipokuwapo, mimi nipo; na sasa Bwana MUNGU amenituma, na roho yake.
17 Bwana, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.
18 Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari;
19 Tena wazao wako wangalikuwa kama mchanga, na hao waliotoka katika tumbo lako kama chembe zake; jina lake lisingalikatika, wala kufutwa mbele zangu.
Kijana na uchumi katika zama za utandawazi;
Nabii Isaya anakiri kutumwa na Mungu, akileta ujumbe kuwa Bwana ndiye afundishaye watu ili waishike njia iwapasayo, waifuate. Isaya analeta ujumbe wa watu kushika amri za Mungu ili wawe na amani. Isaya anasisitiza kuwa hakuna amani kwa wasioishika sheria ya Bwana.
Ni wito wa kuzishika amri za Mungu siyo kwa vijana tu, bali kwa Kanisa lote la Kristo. Tukizishika amri zake ndipo tunakuwa na amani katika yeye, tukitenda yatupasayo kwa utukufu wake. Shika amri za Mungu, fanya kazi kwa bidii. Acha uvivu.
Uwe na wiki njema.