Date: 
30-03-2023
Reading: 
Hesabu 21:4-9

Hii ni Kwaresma 

Alhamisi asubuhi tarehe 30.03.2023

Hesabu 21:4-9

4 Wakasafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia ya Bahari ya Shamu; ili kuizunguka nchi ya Edomu, watu wakafa moyo kwa sababu ya ile njia.

5 Watu wakamnung'unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu.

6 Bwana akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa.

7 Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa Bwana, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu.

8 Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi.

9 Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.

Yesu ni mpatanishi;

Wana wa Israeli walimlalamikia Musa ni kwa nini aliwatoa Misri, maana wakiwa njiani walikosa chakula kama walichokula wakiwa kule utumwani. Mungu alituma nyoka wakawauma, wengi walikufa. Musa aliwaombea, Mungu akamwambia kutengeneza nyoka wa shaba, na kila aliyemtazama huyo nyoka aliishi. Hapa Musa alifanya upatanisho kati ya Israeli na Mungu.

Yohana anarejea tukio hili kama upatanisho wakati wa Agano la kale, akimtambulisha Yesu Kristo kama Mpatanishi wetu na Mungu;

Yohana 3:14-16

14 Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;
15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Yesu ndiye Mpatanishi wetu na Mungu. Tusipomwamini tumepotea, bali tukimwamini na kumfuata ametuahidi uzima wa milele.

Alhamisi njema 

 

Heri Buberwa