Ibada za Krismasi 2023 | Usharika wa Azania Front Cathedral
Katika ibada ya mkesha wa Krismasi (Usiku Mtakatifu), siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa mwokozi Yesu Kristo iliyofanyika tarehe 24/12/2023 kwenye Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front na kuongozwa na Msaidizi wa Baba Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dean Chediel Lwiza, washarika kuwa na imani na Mungu kwa kuiga mfano wa Bikira Maria ambaye alipewa habari ya uzao wa Yesu Kristo na akaamini.