Ibada zote LIVE Azaniafront TV

Mpendwa msharika na watu wote wa Mungu, kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, sasa ni dhahiri kwamba unaweza kushiriki kikamilifu katika ibada zetu zote ukiwa sehemu yoyote duniani.

Ungana nasi katika ibada zote za kila siku za wiki, pamoja na ibada kuu za siku ya Jumapili kwa kufuatilia matangazo ya moja kwa moja (LIVE) kupitia chaneli yetu ya Youtube ya AZANIAFRONT TV

Subscribe kwenye chaneli hiyo ili uweze kupata taarifa (notification) kila kunapokuwa na jambo linaendelea usharikani. 

Karibu Azaniafront Cathedral, Tumwabudu Mungu Pamoja

Usharika wa KKKT Kanisa Kuu Azaniafront Cathedral unawakaribisha watu wote katika ibada zake za kila siku za Jumapili, pamoja na ibada za katikati ya wiki. 

Usharika unawakumbusha washarika pia kuchukua tahadhari za Covid-19 wawapo kanisani.

Pia washarika wanaweza kushiriki katika ibada zote zinazofanyika usharikani wakiwa popote duniani kupitia chaneli ya Youtube ya AZANIAFRONT TV. Ibada zote zinakuwa LIVE.

Mungu awabariki wote.