Date: 
24-02-2021
Reading: 
James 1:1-4 (Yakobo 1:1--4)

WEDNESDAY 24TH FEBRUARY 2021, MORNING                                      

James 1:1-4 New International Version (NIV)

Temptations and trials are to strengthen our faith in Christ.

1 James, a servant of God and of the Lord Jesus Christ,

To the twelve tribes scattered among the nations:

Greetings.

Consider it pure joy, my brothers and sisters,[a] whenever you face trials of many kinds, because you know that the testing of your faith produces perseverance. Let perseverance finish its work so that you may be mature and complete, not lacking anything.

In order to receive the benefits of maturing through our trials, we must first acknowledge that God has put them there, or allowed them to be there, for our benefit.  If we miss that, we miss the opportunity to grow.

The devil wants to use trials to discourage us, to weaken us, to turn us against one another; but God wants to use them to strengthen us, to complete us, and to make us the church of Jesus, pure and undefiled!

Our trials lead to endurance, which leads to maturity.  However, we will never be perfect on this earth.

We are on a journey each day to become sanctified, to be made Holy; each day becoming more and more like Jesus.


JUMATANO TAREHE 24 FEBRUARY 2021,  ASUBUHI                        

YAKOBO 1:1-4

Majaribu yapo kuimarisha Imani yetu katika Yesu Kristo.

Yakobo, mtumwa wa Mungu, na wa Bwana Yesu Kristo, kwa kabila kumi na mbili waliotawanyika; salamu.
Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;
mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.
Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.

Ili kuona faida za kukua kupitia majaribu, ni lazima kwanza tukubali kuwa Mungu ameyaweka au kuyaruhusu kuwepo kwa faida yetu. Tusipolifahamu hilo, tunakosa fursa ya kukua kiroho.

Shetani anataka kutumia majaribu kutukatisha tamaa, kutudhoofisha na kutugombanisha; lakini Mungu anapenda kutumia majaribu kutuimarisha, kutukamilisha, na kutufanya kuwa kanisa halisi la Yesu lisilo na hila.

Katika majaribu tunapewa kuvumilia, na baadaye kuwa watimilifu. Hata hivyo, hatuwezi kuwa wakamilifu hapa duniani.

Kila siku tuko katika safari ya utakaso, kufanywa watakatifu; ili kila siku, zaidi na zaidi tuzidi kufanana na Yesu.