Date: 
01-11-2022
Reading: 
Yohana 5:30-38

Jumanne asubuhi  tarehe 01.11.2022

Yohana 5:30-38


[30]Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.
[31]Mimi nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli.
[32]Yuko mwingine anayenishuhudia; nami najua ya kuwa ushuhuda wake anaonishuhudia ni kweli.
[33]Ninyi mlituma watu kwa Yohana, naye akaishuhudia kweli.
[34]Lakini mimi siupokei ushuhuda kwa wanadamu; walakini ninasema haya ili ninyi mpate kuokoka.
[35]Yeye alikuwa taa iwakayo na kung’aa, nanyi mlipenda kuishangilia nuru yake kwa muda.
[36]Lakini ushuhuda nilio nao mimi ni mkubwa kuliko ule wa Yohana; kwa kuwa zile kazi alizonipa Baba ili nizimalize, kazi hizo zenyewe ninazozitenda, zanishuhudia ya kwamba Baba amenituma.
[37]Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamkuiona.
[38]Wala neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwa kuwa ninyi hammwamini yule aliyetumwa na yeye.

Ushuhuda wetu; Hapa nimesimama;

Yohana anaandika jinsi Yesu alivyojishuhudia kuwa yeye alikuwa anatenda iliyo haki, akitoka mbinguni kwa Baba. Yesu alikiri kuwa ushuhuda wake ni mkuu kuliko Yohana, maana kazi alizotumwa zilimshuhudia kwamba alitumwa na Baba. Yesu alionesha kufanya katika Utatu Mtakatifu akijishuhudia kama Mungu wa kweli.

Ushuhuda wa Yesu ulilenga kuonesha kuwa yeye aliihubiri kweli iliyotoka mbinguni. Na kwa ushuhuda huo alitaka watu wamwamini na kumpokea. Hatuwezi kusimama katika Imani kama hatujaishi kwa neno la Kristo ambalo ndilo ushuhuda unaoishi.


Siku njema.