Event Date: 
12-06-2015

Usharika wa Azania Front ulipokea ugeni kutoka usharika wa Messiah jimbo la Marquete, Michigan nchini Marekani, waliofika tarehe 12/6/2015 na kuondoka 22/6/2015.

Messiah ni Usharika rafiki na usharika wa Azania Front toka miaka ya 90, sharika hizi zimekuwa zikishirikiana kwa ukaribu kabisa hasa katika tamaduni za kutembeleana huku wakiwa na kauli mbiu moja ya kutangaza injili.

Wangeni walifanikiwa kutembelea maeneo mbalimbali yanayohusina na kanisa la KKKT pia kutembelea maeneo ya makumbusho Daresalaam na Bagamoyo, na baadae mbuga za wanyama za Tarangire na Serengeti.

Wageni hawa walifanikiwa kukutana na vikundi mbalimbali vinavyotoa huduma usharikani Azaniafront kama kwaya, madarasa ya Sunday School ,Pia walifanikiwa kukutana na watu mbalimbali na kubadilishana mawazo kuhusu Neno la mungu sambamba na kushiriki ibada ya nyumba kwa nyumba.

wamarekani wa messiah01

Vijana Lisa (Kushoto) na Courtney wakifurahia jambo katika ibada ya kwanza.

wamarekani wa messiah02

Mama Elipina Mlaki (kulia) akitoa maelekezo kuhusu darasa la kiswahili la shule ya Jumapili

wamarekani wa messiah03

Mch. Dave Mckenly akishukuru kwa zawadi ya Biblia kubwa aliyokabidhiwa kwa niaba ya Usharika.

wamarekani wa messiah04

Mchungaji Dave akikabidhi zawadi kwa Mwl. Jane Mhina kwa ajili ya watoto wa darasa la kiswahili la shule ya jumapili.

wamarekani wa messiah05

Mch. Dave akionyesha zawadi ya msalaba wa shanga uliotengenezwa na watoto wa Sunday School ya Messiah.

wamarekani wa messiah06

Mchungaji kiongozi wa wageni akiongoza wageni kuwaaga washarika wa Azania Front

wamarekani wa messiah07

Mchungaji kiongozi wa wageni kutoka Usharika wa Messiah Michigan Marekani akifuatilia ibada

wamarekani wa messiah08

Mchungaji mgeni akimuonyesha zawadi mchungaji Mzinga

wamarekani wa messiah09

Mchungaji mgeni akimvisha zawadi ya Skafu Mchungaji Mzinga

wamarekani wa messiah10

Mchungaji mgeni akionyesha zawadi ya Biblia washarika wa Azania Front. Nyuma yake ni Jito, na Mzee George Mnyitafu mwanakamati wa

Uhusiano.

wamarekani wa messiah11

Mchungaji mgeni akisoma neno la shukrani kwa washarika wa Azania Front.

wamarekani wa messiah12

Mchungaji Mzinga akimkabidhi mchungaji mgeni zwadi ya picha ya kanisa baada ya hafla ya chakula cha mchana siku ya kuagana.

wamarekani wa messiah13

Mchungaji Mzinga akimkabidhi mgeni zawadi ya Biblia ya kiswahili. Kulia ni Balozi Bertha Somi, mwanakamati ya Uhusiano.

wamarekani wa messiah14

Chaplain Mzinga akikabidhi moja ya vitabu vya Historia ya miaka mia ya Usharika kwa Mch. Dave kwa niaba ya wageni.

wamarekani wa messiah15

Mchungaji Mzinga akishiriki chakula cha mchana pamoja na wageni

wamarekani wa messiah16

Baadhi ya wenyeji wa wageni nao walishiriki chakula cha Mchana

wamarekani wa messiah17

Mchungaji Mzinga na mzee Swai wakionyesha zawadi ya picha ya jengo la kanisa wageni kabla ya kukabidhiwa

wamarekani wa messiah18

Mgeni akionyesha ishara ya kanisa na watu

wamarekani wa messiah19

Mgeni Lisa akitoa maelezo kuhusu zawadi kwa usharika. Kati ni Katelin, akifuatiwa na Courtney. Nyuma yao ni Prof. Carol.

wamarekani wa messiah20

Mwalimu Stella na watoto wa darasa la kiingereza wakiimba pamoja na wageni walipopita kuwasalimia.

wamarekani wa messiah21

Mwalimu Stella akitoa maelezo kuhusu darasa la kingereza ibada ya asubuhi

wamarekani wa messiah22

Mwanakamati ya Uhusiano, Mama Aida (Kushoto) akishiriki chakula cha mchana pamoja na wageni

wamarekani wa messiah23

Mwanakamati wa Uhusiano mama Aida Mwakisu akiwa katika picha ya pamoja na mgeni

wamarekani wa messiah24

Mzee Swai, Katibu wa kamati ya Uhusiano, akiwa na wageni katika kikao cha mrejesho na wageni.

wamarekani wa messiah26

Mzee Swai akiwa na wageni wakielekea katika madarasa ya sunday school

wamarekani wa messiah27

Kulia ni David Blomquist akifatiwa na Aaron Ndasiwa, aliyekuwa akitafsiri, mwisho ni Mary Lou Blomquist

wamarekani wa messiah28

Wageni wakifurahia chakula cha mchana

wamarekani wa messiah29

Mwl. Mgana (kulia) akiwakaribisha wageni kushiriki zawadi kidogo toka kwa watoto wa darasa la Kiingereza.

wamarekani wa messiah30

Wageni wakiimba na watoto darasa la Kiingereza.

wamarekani wa messiah31

Wageni wakionyesha moja ya zawadi walizotoa kwa usharika. Aliye kushoto ni Mark Paulsen, na kulia ni Prof. Carol

wamarekani wa messiah32

Wageni wakionyesha Ramani ya kanisa lao lilipo huko Michigan, Marekani. kulia ni Dr. David Luoma

wamarekani wa messiah34

Wageni wakisalimia na na walimu wa darasa la kiswahili

wamarekani wa messiah35

Wageni wakishiriki ibada ya Pili. Mwenyeji anayeonekana ni Mzee Elibariki Moshi.

wamarekani wa messiah36

Wageni wakifurahi na watoto wa shule ya Jumapili

wamarekani wa messiah37

Wageni wakitoa baadhi ya zawadi kwa watoto.

wamarekani wa messiah38

Wageni wakiwa katika darasa la kingereza ibada ya asubuhi

wamarekani wa messiah39

wamarekani wa messiah40

Wageni wakiwa na wenyeji katika chakula cha mchana

wamarekani wa messiah41

wamarekani wa messiah42

Wageni wakiimba na watoto

wamarekani wa messiah43

Wageni wakisaliamiana na waalimu wa darasa la Kiswahili

wamarekani wa messiah44

Wanakamati wa kamati ya Uhusiano wakipokea zawadi za usharika kwaniaba ya washarika

wamarekani wa messiah45

Darasa la shule ya jumapili la kiswahili wakiwaimbia wageni.

wamarekani wa messiah46

Watoto wakioneshwa zawadi yao ya msalaba kutoka kwa watoto wa Usharika wa Messiah Marekani

wamarekani wa messiah47

Watoto wakipokea zawadi yao ya msalaba uliotengenezwa na watoto wenzao wa Marekani.

wamarekani wa messiah48