Umoja wa wanawake Azania Front wakiongozwa na Mwenyekiti wa umoja huo Apaisaria Kilewo uliofuatana na Mama Askofu Erica Malasusa, walitembelea kituo cha kulelea watoto yatima na watoto wenye mazingira hatarishi cha DonBosco kilichopo Kimara Suka Dar es salaam. Mama Erika Malasusa alitoa neno la ufunguzi wa maongezi mafupi kati ya umoja wa wanawake na watoto wa kituo hicho pamoja na uongozi wa kituo hicho, Neno lilitoka katika kitabu cha Yohana 13: 34-35 Kituo cha Don Bosco kilianzishwa mwaka 1998, na Evans Tegete, ambaye ndio mkurengenzi wa kituo hicho, mpaka sasa kituo kina watoto wasiopungua 88 wa rika mbalimbali. Kituo hiki ni kutuo pekee ambacho kimekuwa kikisimamia maadili kwa watoto ambao wanaishi katika kituo hicho, mpaka sasa kituo kimesomesha wanafunzi 26 ambao wamemaliza ngazi ya chuo kikuu, mbali na hao kuna wanafunzi 21 ambao bado wanaendea na chuo pia kuna wanafunzi 9 ambao wako kidato cha nne na cha tano. Mbali na umoja wa wanawake kupeleka zawadi za sikukuu kama mchele, sukari, mafuta, mikate,sabuni, majani ya chai chumvi n.k . pia umoja huo unasomesha wanafunzi saba wa ngazi ya Sekondari na chuo. Mkurugenzi wa kituo hicho aliushukuru umoja huo kwa kusema kwamba bila wakina mama hawa asingeweza kufika hapo alipofiki kwasababu wamekuwa wakimtia sana moyo na kumuombea ili aendelehe kuwatunza watoto wenye uhitaji. ”Bila kinamama wa Azania Front naisi hiki kituo kisinge wepo tena maana wakinamama hawa wamekuwa wakinapa sapoti kubwa sana ambayo sikutegemea kabisa lakini kwa uwezo wa Mungu wakinamama wameweweza kunitia moyo na kunisaidia kwa namna mbalimbali kama kuniletea misaada kuwasomesha baadhi ya watoto katika ngazi tofautitofauti nawashukuru sana ninawaombea kwa Mungu muendelee kushikamana na umoja wa kina mama huo wa Azaniafront udumu milele” |
Baadhi ya Vijana ambao wanaosomeshwa na kituo hicho
Baadhi ya watoto ambao wako kidato chja tano wakinyoosha mikono juu
Baadhi ya watoto na wakinamama wa azania front wakiwa wanasikiliza jambo kwa makini
Hili ni jengo la kituo cha Don Bosco
Katibu, mama msangi akifurahia jambo na mtoto
Kijana wa kituo cha Don Bosco akisukuru kwa niaba ya wanzake ujio wa umoja wa
wanawakeÂÂÂÂÂÂÂ kwa zawadi za christmas na kuwatembelea
Mama Apaisalia kilewo akifurahia jambo
Mama Apaisalia KIlewo akisema jambo kwa watoto wa kituo cha Don Bosco
Mama askofu Erica Malasusa akiandaa somo, kushoto ni Elly Swai na kulia ni Hilda
RwanshaneÂÂÂÂÂÂÂ
Mama askofu Erica Malasusa akifunga kwa sala
Mama Askofu Erica Malasusa akifungua kwa salaÂÂÂÂÂÂÂ
Mama Askofu Erica Malasusa akitoa neno kwa watoto wa kituo cha Don Bosco na umoja
wa wanawake Aania Front
Mkurugenzi wa kituo cha Don Bosco Evance Tegete akiwakaribisha wakinamama wa
Azania Front
Mkurugenzi wa kituo cha Don Bosco MR Evance Tegete akibadilisha jambo na katibu
Theuda msangi na mjumbe wa umoja wa wanawake Azania Front
Nsarry hoza msimamizi wa watoto wanafunzi akito shukrani kwa niaba ya uongozi wa
kituo
Umoja wa kinamama wakiwasili katika kituo cha Don Bosco
Vijana ambao wanaingia kidato cha kwanza mwakani
Zawadi za christmas ambazo watoto wameletewa na umoja wa kinamama Azania Front