Date: 
02-02-2021
Reading: 
Romans 3:21-26

TUESDAY 2nd FEB 2021

Romans 3:21-26 (NIV)

Righteousness Through Faith

21 But now apart from the law the righteousness of God has been made known, to which the Law and the Prophets testify. 22 This righteousness is given through faith in[a] Jesus Christ to all who believe. There is no difference between Jew and Gentile, 23 for all have sinned and fall short of the glory of God, 24 and all are justified freely by his grace through the redemption that came by Christ Jesus. 25 God presented Christ as a sacrifice of atonement,[b] through the shedding of his blood—to be received by faith. He did this to demonstrate his righteousness, because in his forbearance he had left the sins committed beforehand unpunished— 26 he did it to demonstrate his righteousness at the present time, so as to be just and the one who justifies those who have faith in Jesus.


JUMANNE TAREHE 2 FEBUARI 2021

WARUMI 3:21-26 (SNT)

Haki Kwa Njia Ya Imani

21 Lakini sasa, njia ya Mungu ya kuwahesabia watu haki pasipo sheria, njia ambayo sheria na manabii huishuhudia, imekwisha dhihirishwa. 22 Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa kumwamini Yesu Kristo. Mungu huwatendea hivi watu wote wamwaminio Kristo pasipo kubagua, 23 kwa maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 24 wote wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa ukombozi ulioletwa na Yesu Kristo. 25 Mungu alimtoa awe dhabihu ya upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alifanya hivi ili kuonyesha haki yake, kwani kwa uvumilivu wake hakuziadhibu dhambi za zamani. 26 Pia alifanya hivi ili kuonyesha kwa wakati huu kuwa yeye ni wa haki na kwamba yeye ndiye anayewahesabia haki watu wote wamwaminio Yesu.