DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 05 JULAI, 2026
SIKU YA BWANA YA 5 BAADA YA UTATU
SIKUKUU YA VIJANA
NENO LINALOTUONGOZA LEO NI:
“KANISA NI MSINGI WA MALEZI BORA”
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Leo ni sikukuu ya vijana hivyo Ibada itaongozwa na Vijana.
3. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia na cheti: Kama kuna wageni ambao ni mara yao ya kwanza kushiriki nasi wasimame ili tuwakaribishe.
4. Matoleo ya Tarehe 28/06/2026
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
5. Mahudhurio ya ibada za tarehe 28/06/2026 ni Washarika 711 na Sunday School 180
6. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4 :30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
7. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
8. Jumapili ijayo tarehe 12.07.2026 katika ibada ya pili familia ya Dr. na Bibi Donald Mmari watamshukuru Mungu kwa kufikisha miaka 30 ya Ndoa.
Neno: Zaburi 116:12-14, wimbo 708 Mission Praise.
9. NDOA. Ndoa za washarika
KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 18/07/2026
SAA 9.00 ALASIRI
-
Bw. Erick Richard Mtega na Bi. Dorina Nelson Zachwa
KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 11/07/2026
SAA 7.00 MCHANA
-
Bw. Erick godfrey Kimaro na Bi. Liben Geuken Mmary
SAA 9.00 ALASIRI
-
BW. Christopher Kelvin Chambo na Bi. Gillian Hope Mlowe
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
10. BARAKA YA MTOTO
Familia ya Emmanuel Alexandre na Sania Kasyanju wamepata Baraka ya mtoto wa kike tar 28/06/2026 Hospital ya Aghakhani Mama na mtoto wanaendelea vizuri.
11. Uongozi wa Usharika unapenda kuwashukuru jumuiya zote Pamoja na msharika mmoja mmoja kwa kufanikisha kambi ya
Watoto Morogoro Mungu awabariki kwa sadaka yenu njema.
12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Mjini kati: kwa Elisifa Ngowi
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa mama Mamkwe
- Kinondoni: Kwa Danford Mariki
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Allen David
- Upanga: Kwa Bi Agness Mziray
13. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
14. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la kwanza
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.
