Jumatano asubuhi tarehe 19.11.2025
Ufunuo wa Yohana 20:11-15
11 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Jiandae kwa hukumu ya mwisho;
Asubuhi ya leo tunamsoma Yohana akifunuliwa kiti cha enzi kikubwa, cheupe, lakini mbingu na nchi zinakimbia uso wa aketiye kwenye kiti! Huyu ni Mungu mwenye utukufu, tayari kwa hukumu. Yohana anaoneshwa wafu wakubwa kwa wadogo wakiwa wamesimama mbele ya kiti hicho, kitabu cha uzima kinafunguliwa na kila mmoja anahukumiwa sawasawa na matendo yake.
Yohana anatukumbusha kwamba hukumu ya mwisho ipo, alifunuliwa ili kutuonesha sisi yajayo. Mstari wa 15 uko wazi kwamba mtu yeyote ambaye hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika ziwa la moto. Ndivyo itakavyokuwa, kwamba wote waliompokea Bwana wetu Yesu Kristo na kumwamini, wakaishi kwa kadri ya mapenzi yake, wataurithi uzima wa milele. Basi fanya hivyo, yaani mwamini Yesu ukijiandaa kwa hukumu ya mwisho. Amina
Jumatano njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650
