Date: 
28-10-2025
Reading: 
2 Wafalme 23:25-25

Jumanne asubuhi tarehe 28.10.2025

2 Wafalme 23:24-25

24 Tena wenye pepo wa utambuzi, na wachawi, na vinyago, na sanamu, na machukizo yote yaliyoonekana katika nchi ya Yuda na katika Yerusalemu, Yosia akayaondoa yote, ili apate kuyathibitisha maneno ya torati yaliyoandikwa katika kile kitabu alichokiona Hilkia kuhani ndani ya nyumba ya Bwana.

25 Kabla ya huyo hapakuwa na mfalme mfano wake, aliyemwelekea Bwana kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, na kwa nguvu zake zote, sawasawa na sheria zote za Musa; wala baada yake hakuinuka mmoja mfano wake yeye.

Ushuhuda wetu;

Ondoa yaliyo chukizo mbele za Mungu;

Mfalme Yosia katika mwaka wake wa kumi na nane wa kutawala anafanya Matengenezo katika nyumba ya Mungu wakati wa Pasaka. Yosia anaondoa pepo wa utambuzi, wachawi, vinyago, sanamu n.k Yosia alifanya hivi ili apate kuyathibitisha maneno ya torati yaliyokuwa yameandikwa katika kitabu kilichokuwa kimeonekana na Hilkia Kuhani ndani ya nyumba ya Bwana.

Maandiko yanasema kabla ya huyo Yosia hapakuwa na mfalme mfano wake aliyemwelekea Bwana kwa moyo wake wote, kwa roho yake yote, kwa nguvu zake zote sawasawa na sheria ya Musa. Yosia anatutafakarisha kumrudia Bwana anapoisafisha nyumba ya Mungu. Tutubu dhambi zetu, Yesu yuaja. Amina

Jumanne njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com