Date: 
29-01-2025
Reading: 
Marko 1:32-34

Hii ni Epifania 

Jumatano asubuhi tarehe 29.01.2025

Marko 1:32-34

32 Hata kulipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, walikuwa wakimletea wote waliokuwa hawawezi, na wenye pepo.

33 Na mji wote ulikuwa umekusanyika mlangoni.

34 Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua.

Mungu hana upendeleo;

Yesu alikuwa ameanza huduma yake akihubiri, kufundisha na kuponya. Ukisoma nyuma kidogo, unaona akimponya mwenye pepo mchafu (21-28). Baadaye anamponya mkwe wake Simoni ambaye alikuwa hawezi kitandani. Ndipo linakuja somo la asubuhi hii, Yesu akiwa hapo kwa Simoni analetewa wagonjwa wengi wenye pepo na ambao walikuwa hawawezi, akawaponya.

Somo linaonesha Yesu akiponya watu wote walioletwa mbele yake. Hakuwabagua, hakuonesha upendeleo. Yesu yuko hivyo hata sasa, hana upendeleo. Wajibu wetu ni kumpokea akae mioyoni mwetu, lakini nasi tukiiga mfano wake wa kutokuwa na upendeleo. Tumwamini asiye na upendeleo kwa kuishi bila upendeleo. Amina

Jumatano njema

Heri Buberwa