Date: 
23-01-2025
Reading: 
Yakobo 3:13-18

Hii ni Epifania 

Alhamisi asubuhi tarehe 23.01.2025

Yakobo 3:13-18

13 N'nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.

14 Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli.

15 Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani.

16 Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.

17 Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.

18 Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.

Mungu hubariki nyumba zetu;

Bwana Asifiwe;

Yakobo anaandika juu ya aina mbili za hekima. Anasema kwamba hekima ya mtu huonekana kwa mwenendo mzuri. Watendao mabaya kama vile wivu, uongo, kutopenda haki n.k wana hekima isiyotoka kwa Mungu bali ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, ya shetani. Hiyo ni hekima ya kwanza. Hekima ya pili ni ile itokayo juu, ambayo huongoza mtu kutenda yapasayo katika imani.

Yakobo anatuongoza asubuhi hii kuishi kwa hekima itokayo kwa Mungu. Anatuasa kwamba hekima itokayo juu ni ya amani, upole, rehema, upendo n.k. Matokeo ya hekima itokayo juu ni kuishi kwa kutenda yaliyo mapenzi ya Mungu maana mtu huwaza, hunena na kutenda kwa usahihi. Tukiwa na hekima itokayo kwake Kristo, tutaishi inavyompendeza, naye atazibariki nyumba zetu. Amina.

Alhamisi njema

Heri Buberwa