Date:
05-11-2024
Reading:
Wafilipi 7:13-21
Jumanne asubuhi tarehe 05.11.2024
Wafilipi 3:17-21
17 Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi.
18 Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;
19 mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.
20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;
21 atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.
Sisi ni wenyeji wa mbinguni;
Mtume Paulo anawaambia Wafilipi kumfuata yeye na wale waendao kwa mfano wa mafundisho yake. Paulo hapa hakuwataka kumfuata yeye, bali waishi kwa kufuata Injili kama alivyoihubiri. Anawataka kuwaepuka wote ambao hufundisha kinyume na Injili ya Kristo, ambao mungu wao ni tumbo, maana utukufu wao u katika fedheha yao.
Ujumbe wa Paulo ni kusimama katika Injili ya kweli. Anatutaka kusimama katika Injili ya kweli maana sisi ni wenyeji wa mbinguni. Maisha yetu yawe ya kumtazama Kristo atuingizaye katika Utukufu wake. Tuitikie wito wa Paulo kwa kutubu na kuiamini Injili, maana uenyeji wetu ni wa mbinguni. Amina
Jumanne njema
Heri Buberwa