MATANGAZO YA USHARIKA  

TAREHE 22 SEPTEMBA, 2024

SIKU YA BWANA YA 17 BAADA YA UTATU 

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

UCHAGUZI WAKO NDIYO MAISHA YAKO 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 15/09/2024

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

5. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya shilingi 40,000/= 

6. Tarehe 06/10/2024 itakuwa ni sikukuu ya mavuno. Washarika tujiandae na kuiombea siku hiyo. Sare itakuwa ni kitenge chetu cha Kiharaka.

7. Jumapili ijayo tarehe 29/09/2024 itakuwa ni sikukuu ya mikaeli na watoto. Ibada zote zitaongozwa na watoto. Washarika tuiombee siku hiyo. Aidha Jumamosi ijayo tarehe 28/09/2024 Watoto watakuwa na michezo mbalimbali hapa Usharikani kuanzia saa 3.00 asubuhi.

8. Uongozi wa umoja wa vijana wananapenda kutoa shukrani kwa uongozi wa kanisa,pamaoja na washarika wote kwa kuwawezesha kuhudhuria kwenye makongamano yote mawili la Dodoma na Arusha. Wameenda salama na wamerudi salama. Mungu awabariki wote

9. Shukrani: Jumapili ijayo tarehe 29/09/2024 katika ibada ya tatu saa 4.30 asubuhi.

10. Familia ya Mhe. Freeman Mbowe itatoa sadaka kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyowatendea ikiwa ni pamoja na Dr. Lillian Mbowe kutimiza miaka 60 siku hiyo.

Neno: Zab. 71: 17-18.,Wimbo TMW 149 (Chini ya Bawa lako), Kwaya kuu (Huniongoza Mwokozi)

11. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA 

Hakuna ndoa za Washarika

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu. 

12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Zimba
  • Mjini kati: Itafanyika hapa Kanisani saa 1.00 asubuhi.
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Shanny Mbogolo .
  • Kinondoni: Kwa Profesa G.
  • MmariTegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Philemon Msuya 
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Mch. na Mama Charles Mzinga
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: ……………………………………….. 
  • Oysterbay, Masaki: Kwa Mama Nisile Mollel.

13. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili.  

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.