Date: 
06-09-2024
Reading: 
Zekaria 7:8-10

Ijumaa asubuhi tarehe 06.09.2024

Zekaria 7:8-10

8 Kisha neno la Bwana likamjia Zekaria, kusema,

9 Bwana wa majeshi amesema hivi, ya kwamba, Fanyeni hukumu za kweli, kila mtu na amwonee ndugu yake rehema na huruma;

10 tena msimdhulumu mjane, wala yatima, wala mgeni, wala maskini; wala mtu awaye yote miongoni mwenu asiwaze mabaya juu ya ndugu yake moyoni mwake.

Mpende Jirani yako;

Nabii Zekaria katika sura ya saba anapewa ujumbe na Mungu juu ya hukumu kwa watu wasiomtii. Nabii Zekaria anawaelekeza watu kuishi katika Bwana, wakioneana rehema na huruma. Zekaria anaendelea kuwaambia wasidhulumu wajane, yatima, mgeni wala , maskini. Zaidi ya yote, Zekaria anawataka kila mmoja kutowaza vibaya juu ya mwenzake.

Ujumbe wa Nabii Zekaria ndiyo ujumbe wa Yesu Kristo tunaopewa kuhusu huruma, kutodhulumu wenzetu, kuwajali wajane, yatima na wahitaji. Kristo anatutaka kuwaziana mema kama yeye anavyotuwazia mema. Mwenendo wetu unatakiwa kuwa wenye upendo kwa jirani zetu, na hapo ndipo tutakuwa tumempenda Mungu katika kweli. Huo ndiyo utii wa kweli kwa Mungu. Amina.

Ijumaa njema

Heri Buberwa