Date:
15-05-2024
Reading:
1 Wathesalonike 5:16-24
Jumatano asubuhi tarehe 15.05.2024
1 Wathesalonike 5:16-24
16 Furahini siku zote;
17 ombeni bila kukoma;
18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
19 Msimzimishe Roho;
20 msitweze unabii;
21 jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema;
22 jitengeni na ubaya wa kila namna.
23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
24 Yeye ni mwaminifu ambaye awaita, naye atafanya.
Omba! Mungu anasikia kuomba kwetu;
Mtume Paulo katika sura hii ya mwisho ya waraka wa kwanza kwa Wathesalonike anawaambia juu ya ujio wa Yesu Kristo kwa mara ya pili. Ni kwa sababu hiyo anawausia kutoiacha imani ya kweli katika Kristo kama walivoipokea. Ndipo anawaambia jinsi ya kuenenda ikiwamo kufurahi siku zote, kuomba, kushukuru, kujitenga na ubaya wakidumu katika utakaso kwa njia ya Roho Mtakatifu.
Ujumbe wa Paulo ni kuishi maisha yanayompendeza Mungu. Maisha haya yanawezekana tukikaa katika imani kama tulivyoipokea kwa kumkiri Kristo. Tukiishi maisha ya uchaji tutaufikia mwisho mwema pale Kristo atakaporudi kulichukua Kanisa. Tuombe tukitimiza wajibu wetu ili tuufikie mwisho mwema. Amina.
Jumatano njema
Heri Buberwa