17 Mtu apitaye na kujisumbua kwa ugomvi usio wake; Ni kama mtu ashikaye mbwa kwa masikio yake.
18 Kama mtu mwenye wazimu atupaye mienge, Na mishale, na mauti;
19 Ndivyo alivyo amdanganyaye mwenzake, Na kusema, Je! Sikufanya mzaha tu?
20 Moto hufa kwa kukosa kuni; Na bila mchongezi fitina hukoma.
21 Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, Na kama kuni juu ya moto; Ndivyo mtu mgomvi achocheavyo uadui.
Jirani wetu
Mwandishi wa methali anasema kuwa mtu anayejihusisha na ugomvi usio wake, ni sawa na kumshika mbwa asiye wake masikio. Ni kama mwenye wazimu. Yuko sawa na amdanganyaye mwenzake, akisema ni mzaha!
Mbwa asiye wa kwako ukimshika masikio lazima akushambulie, au ajitetee kwa kukimbia. Ila uwezekano mkubwa ni kukushambulia, yaani unakuwa hatarini. Hivyo kuhangaika na ugomvi usiokuhusu ni kujitafutia kuumia.
Kwa tafsiri nyingine kuhangaika na mambo yasiyoleta upatanisho na jirani zetu ni kupotea. Ndiyo maana tunaelekezwa kukaa kwa pamoja tukipendana ili sote kwa pamoja tuwe na mwisho mwema. Amina.
Jumamosi njema!
--------------------------------------------
Heri Buberwa
Mlutheri