MATANGAZO YA USHARIKA 

TAREHE 2 JULY, 2023

NENO LINALOTUONGOZA NI

AMRI YA UPENDO 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 25/06/2023

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi jioni saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. 

5. Leo tarehe 02/07/2023 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika tujiandae.

6. Kwaya ya Agape wanapenda kuwakaribisha washarika wote na waimbaji wa vikundi vyote kushirikiana nao kwenye maandalizi ya Tamasha la Uinjilisti Pamoja na safari ya Injili Mwanza. Siku za mazoezi ni Jumatano saa 11.00 jioni, Jumamosi saa 6.00 Mchana na Jumapili baada ya ibada ya kwanza.

7. Jumapili ijayo tarehe 09.07.2023 ni siku ya ubatizo wa watoto wadogo na kurudi kundini wenye kuhitaji huduma hii wafike ofisi ya mchungaji

8. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 15/07/2023

NDOA HII ITAFUNGWA KANISA KUU LA MTAKATIFU JOSEPH DAR ES SALAAM

 • Bw. Deogratias Alfred Mboya na Bi. Sianael Obedy Shoo

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 08/07/2023

NDOA HII ITAFUNGWA KKKT USHARIKA RUANDA MBEYA KATI YA

 • Bw. Zuma Samson Sanga na Bi. Atupa Amos Humbu

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.

 9. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

 • Oysterbay na Masaki: Kwa BWANA NA BIBI DAVID MOLLEL
 • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo:  

         Kwa Bwana na Bibi MtungaI

 • lala, Chang’ombe na Buguruni: BW & BI JAMES MONYO 
 • Kinondoni: Kwa Prof. G. Mmari
 • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: - Bw & Bi Adolphe Lawson 
 • Upanga:Kwa Bwana na Bibi Kavuga
 • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Bw & Bi Theophilius Mlaki
 • Tabata: Kwa Mchungaji Kibona
 • English Service: FAMILIA YA MREMA

10. Zamu: Zamu za wazeeni Kundi la Pili.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.