Date:
30-05-2023
Reading:
Isaya 32:15-18
Hii ni Pentekoste
Jumanne asubuhi tarehe 30.05.2023
Isaya 32:15-18
15 hata roho itakapomwagwa juu yetu kutoka juu; hata jangwa litakapokuwa shamba lizaalo sana; nalo shamba lizaalo sana litakapohesabiwa kuwa msitu.
16 Ndipo hukumu itakaa katika jangwa, na haki itakaa katika shamba lizaalo sana.
17 Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima.
18 Na watu wangu watakaa katika kao la amani; na katika maskani zilizo salama, na katika mahali pa kupumzikia penye utulivu.
Roho Mtakatifu msaada wetu;
Nabii Isaya anaiongelea nchi yenye yenye watu yaani Taifa la Mungu wanaoshughulika na shughuli za kila siku kama kilimo, yaani shambani. Inamwagika Roho juu ya nchi ambapo hata shamba lililoko jangwani linatoa mazao mengi. Sasa hukumu itakaa kwenye jangwa, na haki itakaa katika shamba lizaalo sana.
Isaya anatumia lugha ya shamba kuzaa, tena lililoko jangwani kuelezea nguvu ya Roho Mtakatifu katika maisha ya waaminio. Siyo rahisi jangwa kutoa mazao. Lakini kwa Roho wa Mungu inawezekana.
Hiyo ni lugha ya picha, kwamba Roho Mtakatifu hukaa ndani yetu na kutusaidia kuyatenda yote kwa Utukufu wa Mungu. Kama mstari wa 18 unavyosema, tukiwa na Roho Mtakatifu amani ya Mungu inakaa ndani yetu, kinyume chake ni hukumu. Roho Mtakatifu ndiye msaada wetu, tuombe akae kwetu daima.
Siku njema.
Heri Buberwa