Date: 
22-05-2023
Reading: 
Maombolezo 3:52-57

Jumatatu asubuhi tarehe 22.05.2023

Maombolezo 3:52-57

52 Walio adui zangu bila sababu Wameniwinda sana kama ndege;

53 Wameukatilia mbali uhai wangu gerezani, Na kutupa jiwe juu yangu.

54 Maji mengi yalipita juu ya kichwa changu, Nikasema, Nimekatiliwa mbali.

55 Naliliitia jina lako, Bwana, kutoka lile shimo Liendalo chini kabisa.

56 Ukaisikia sauti yangu; usifiche sikio lako Ili usisikie pumzi yangu, kwa kilio changu.

57 Ulinikaribia siku ile nilipokulilia; Ukasema, Usiogope.

Usikie kuomba kwetu;

Yeremia katika sura ya tatu ya Maombolezo anakiri kuona mateso kwa fimbo ya ghadhabu ya Mungu. Lakini katika mateso hayo anakiri kuongozwa na Mungu. Yeremia anaendelea kusema Bwana hatamuacha mwanadamu kamwe, bali atamlinda na kumhurumia daima.

Katika sehemu ya sura ya 3 tuliyosoma kuanzia mstariwa 52, Yeremia anakiri kuwindwa na adui zake, lakini aliliitia jina la Bwana. Bwana alimsikia sauti yake akamwambia "usiogope". Yeremia anaonesha kuwa Bwana alimsikia na kumuokoa;

Maombolezo 3:58-59

58 Ee Bwana umenitetea mateto ya nafsi yangu; Umeukomboa uhai wangu.
59 Umekuona kudhulumiwa kwangu, Ee Bwana; Unihukumie neno langu.

Yeremia anathibitisha ulinzi wa Mungu juu yake. Mungu hakuishia kumlinda, bali alimrehemu. Lakini katika yote Yeremia alimuita Bwana akamuitikia, yaani Bwana alisikia kuomba kwake. Tunaalikwa kuendelea kudumu katika sala, tukiwa na uhakika kuwa Mungu husikia kuomba kwetu. Amina.

Uwe na wiki njema.

 

Heri Buberwa 

Mlutheri