Date: 
10-08-2022
Reading: 
Mathayo 5:17-22

Jumatano asubuhi tarehe 10.08.2022

Mathayo 5:17-22

[17]Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.

[18]Kwa maana, amin,

nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.

[19]Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.

[20]Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

[21]Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.

[22]Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.

Mlango wa kuingia mbinguni;

Yesu anafundisha juu sheria na manabii, pia hasira. Ujio wa Yesu ulikuwa ni kuleta habari njema ya wokovu, na kuiweka vizuri torati. Wakati wa Agano la kale, alichinjwa kondoo kwa ajili ya sadaka. Lakini Yesu ndiye Mwana kondoo aliyekufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu. Yesu huyu ndiye anayezuia watu wake kuchukiana ili kuiepuka Jehanam ya moto.

Yesu anatuelekeza kulisoma na kulishika neno lake huku tukipendana. Mlango wa kuingia mbinguni uko wazi kwake anayemwamini Yesu na kuwapenda jirani zake. Yesu ameweka wazi katika somo la leo asubuhi, kuwa mwisho wa chuki ni jehanamu. Neno la Mungu ndilo lenye hakika ya hatma yetu.

Siku njema