Date: 
16-11-2022
Reading: 
Mathayo 24:36-41

Jumatano asubuhi tarehe 16.11.2022

Mathayo 24:36-41

[36]Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.

[37]Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

[38]Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,

[39]wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.

[40]Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;

[41]wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.

Jiandae kwa hukumu ya mwisho;

Yesu alikuwa anafundisha juu ya kurudi kwake kwa mara ya pili, akiwaambia wanafunzi wake kujiandaa maana hakuna aijuaye siku hiyo ila Baba. Alitoa mfano wa siku za Nuhu, jinsi baadhi walivyopona na baadhi wakaangamia. 

Ukiendelea kusoma unaona kuwa Yesu alitoa suluhisho;

Mathayo 24:42

[42]Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.

Tunapoambiwa kukesha, ni kudumu katika Imani pasipo kuchoka wala kukata tamaa ili Yesu atakaporudi kwa hukumu tuurithi uzima wa milele. Kupata mali na fursa za dunia tukakosa kuurithi uzima wa milele sio sahihi kwetu wakristo. Tumtumikie Mungu tukifurahia maisha yetu, lakini tusisahau kujiandaa kwa hukumu ya mwisho.

Uwe na siku njema.