Date: 
23-04-2022
Reading: 
Matendo 2:22-28

Hii ni Pasaka;

Jumamosi asubuhi tarehe 23.04.2022

Matendo ya Mitume 2:22-28

22 Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;

23 mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua;

24 ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.

25 Maana Daudi ataja habari zake, Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko upande wa mkono wangu wa kuume, nisitikisike.

26 Kwa hiyo moyo wangu ukapendezewa, ulimi wangu ukafurahi; Tena mwili wangu nao utakaa katika matumaini.

27 Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu; Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu.

28 Umenijuvisha njia za uzima; Utanijaza furaha kwa uso wako.

Tembea na Yesu mfufuka;

Leo asubuhi tunasoma mwendelezo wa hotuba ya Petro siku ile ya Pentekoste, akimsimulia Yesu kama Mwokozi aliyekuja akakataliwa na Wayahudi hadi kusulibishwa, lakini Mungu akamfufua. Petro anamtaja Yesu kama Bwana amwezeshaye Mtakatifu kutokuona uharibifu, akiwajaza furaha wamwaminio.

Tunakumbushwa nguvu ya Yesu na ukuu wake kwa ulimwengu, kama Bwana na mwokozi kwa wote wamwaminio na kumpokea. Kufufuka kwake ni udhihirisho wa nguvu yake, lakini ni ushindi wake juu ya dhambi. Tuwe na imani timilifu kwa Yesu Kristo, ili nasi atufufue siku ile ya mwisho.

Siku njema.