MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 23 APRILI, 2017
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI YESU KRISTO AJIFUNUA KWA WANAFUNZI
- Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
- Wageni: wageni waliotufikia na cheti ni Mrs Patricia Namonje Sinyinza toka United Church of Zambia Usharika wa St. Peter’s Mwenzo
- Uongozi wa Umoja wa Wanawake unapenda kuwakumbusha wanawake kuwa tamasha la uimbaji ni tarehe 13.05.2017 mazoezi yanaendelea kila Jumatano saa 10.00 jioni.
- Jumapili ijayo tarehe 30/05/2017 katika ibada ya pili Dada Catherine Jengo atamshukuru Mungu kwa kumlinda kwenye ajali aliyopata na kumponya majeraha yote.
Neno: Zaburi 111:1, Wimbo: Kwaya ya Vijana (Namshukuru Mungu)
- Mzee Salewi anaomba kukutana na wamachame wote baada ya ibada hapo nje chini ya mti.
- Kamati ya Misioni na Uinjilisti kwa niaba ya Uongozi wa Kanisa Kuu Azania Front, inapenda kuwatangazia watu wote kuwa Semina ya NDOA NA FAMILIA kwa siku 9, imeanza jana jumamosi tarehe 22.04.2017 mpaka jumapili tarehe 30.04.2017 kila siku hapa Usharikani Azania Front. Semina hiyo itafundishwa na Mch. Mathias Mushin a Mkewe Jessie Mushi toka KKKT Kaskazini Kati Arusha. Semina hii itahusu watot, vijana na wanandoa wa kila rika. Aidha kutakuwa na muda wa maombi na maombezi.
Ratiba ya Semina ni Kama ifuatavyo:
Jumapili 23 April 2017 saa 9.00 alasiri: ufunguzi wa Semina na siku ya kwanza ya Semina
Jumatatu 24 April 2017 - Ijumaa 28 April 2017 saa 11:30 - 1:00 Vipindi vya Semina kwa wanandoa
Jumatano 26 April 2017 saa 4:00 asubuhi Semina kwa Vijana
Saa 9.00 alasiri Wajane na Wagane
Saa 11.00-1.30Semina ya Wanandoa na wagane na Wajane
Jumamosi tarehe 29 April 2017 saa 4:00 asubuhi
- watoto wote - saa 4.00-5.00
- vijana wote - saa 4.00 – 7.00 mchana
- kwaya zote - saa 5:30
Jumamosi 29 April 2017 - Jumapili 30 April 2017 saa 9:00 - 12:00 Jioni - Semina ya Wanandoa
Jumapili 30.04.2017, kutakuwa na Sherehe ya wanandoa na kukata keki.
Wote mnakaribishwa na muwakaribishe na wengine.
- NDOA
NDOA ZA WASHARIKA
Kwa mara ya Kwanza tunatangaza ndoa za tarehe 13/05/2017
SAA 9.00 ALASIRI
Bw. Erick Godian Mwakipesile na Bi. Adeline Josephine Mmbaga
SAA 10.00 JIONI
Bw. Ajelandro Mushobozi Sindano na Bi. Rehema Mahmoud Kikwere
Kwa mara ya Pili tunatangaza ndoa za tarehe 06/05/2017
SAA 6.00 MCHANA
Bw. Morries Walter Shangali na Bi. Elke Norah Sumari
SAA 10.00 JIONI
Bw. Eliah Emmanuel Kinyunyu na Bi. Emilia Bonifas Mdamba
Kwa mara ya Tatu tunatangaza ndoa za tarehe 29/04/2017
SAA 9.00 ALASIRI
Bw. Edson Kakulu Ndanguzi na Bi. Gloria Nomsa Labarani
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.
- Ibada za Nyumba kwa Nyumba
- Upanga: kwa Bwana na Bibi Kisamo
- Kinondoni: Watatangaziana
- Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Dk na Bibi David Ruhago
- Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Watatangaziana
- Oysterbay/Masaki: Watatangaziana
- Tabata: Watatangaziana
- Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Mama Korosso
- Mjini kati: Watatangaziana
- Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Watatangaziana
Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Kwanza.
Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.
ZAMU ZA WAZEE
IBADA I
Mzee N. Ndosa - Neno: Zab. 115:1-10, 1Kor. 15:12-19, Yn: 20:26-29
Mzee N. Masawe - Matangazo
Mzee V. Minja - S/School
Mzee S. Jengo - Ndoa
IBADA II
Mzee Doris Maro - Neno: Zab. 115:1-10, 1Kor. 15:12-19, Yn: 20:26-29
Mzee V. MPuya - Matangazo
Mzee E. Mlaki - S/School
Mzee E. Nangawe - Ndoa