Date: 
02-02-2022
Reading: 
Marko 4:35-41

Jumatano asubuhi tarehe 02.02.2022

Marko 4:35-41

35 Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo.

36 Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye.

37 Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji.

38 Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?

39 Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.

40 Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado?

41 Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?

Tunalindwa na nguvu za Mungu;

Wanafunzi wakiwa baharini chombo kilianza kuyumba wakawa kwenye hatari ya kuzama. Yesu alikuwa amelala ikabidi wamwamshe. Yesu aliukemea upepo bahari ikatulia.

Yesu alikuwa mwanadamu kweli na Mungu kweli. Hivyo alikemea upepo kwa mamlaka kama Mungu kweli. Kwa maana hiyo Mungu aliwaokoa wanafunzi wasizame baharini. Walipozidiwa walimwamsha Yesu. Walilindwa na nguvu za Mungu. Usisubiri kuzidiwa ndipo umwamshe Yesu. Mruhusu awe kwako, na nguvu yake ikae kwako ili usizame, usiangamie.

Uwe na siku njema.