Date: 
11-07-2022
Reading: 
Luka 6:6-11

Jumatatu asubuhi tarehe 11.07.2022

Luka 6:6-11

6 Ikawa siku ya sabato nyingine aliingia katika sinagogi akafundisha; na mlikuwamo mtu ambaye mkono wake wa kuume umepooza.

7 Na waandishi na Mafarisayo walikuwa wakimvizia, ili waone kwamba ataponya siku ya sabato; kusudi wapate neno la kumshitakia.

8 Lakini yeye akayatambua mawazo yao, akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, Ondoka, simama katikati; akaondoka akasimama.

9 Ndipo Yesu akawaambia, Nawauliza ninyi, Je! Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya; kuponya roho au kuangamiza?

10 Akawakazia macho wote pande zote, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena.

11 Wakajawa na uchungu, wakashauriana wao kwa wao wamtendeje Yesu.

Mungu ni mwingi wa huruma na haki;

Yesu alimponya mtu aliyepooza mkono siku ya sabato, jambo ambalo halikuwafurahisha kabisa Waandishi na Mafarisayo, maana ilikuwa kinyume na taratibu. Yesu alimwonea huruma aliyepooza mkono, akamponya, hakuangalia taratibu za Wayahudi. 

Wakati Waandishi na Mafarisayo wakitafuta jinsi ya kumtenda Yesu aliyevunja sheria ya sabato, yeye alijawa na huruma kuponya watu. Huruma hii bado ipo leo, ambayo kwake tumeokolewa. Yesu mwenye huruma anatuita kumwendea kwa imani tukimwamini na kumfuata, ili atupe uzima wa milele.

Yesu wa huruma na haki akutangulie.

Wiki njema.