Event Date:
01-04-2019
Jumapili ya tarehe 24/03/2019 Kwaya Kuu ya Kanisa Kuu la Azania Front ili fanya Uzinduzi wa Kanda yake ya Kwanza ya DVD yenye nyimbo 10 yenye jina la SIKU MOJA ILIYOBADILI MAISHA YANGU. Uzinduzi huo ulifanywa na Mch Charles Mzinga kwa niaba ya Baba Askofu Alex Gehazi Malasusa. Kwaya hii imeshatoa kanda za Audio/CD tisa. DVD hii imetokana na kanda ya CD ya tisa yenye jina hilo hilo. Kwaya hii ilianza mwaka 1950 na Ina miaka 69 sasa. Mgeni Maalumu katika Uzinduzi huo alikuwa Mhe Edward Ngoyai Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uzinduzi George Israel Mnyitafu akijadiliana jambo na Mchungaji Kiongozi.
Mwenyekiti wa Kwaya Bw Elisha Mushumbusi akitoa maelezo mafupi kuhusu DVD hiyo.
Mwenyekiti wa Kwaya Bw Elisha Mushumbusi akimkabidhi DVD Mgeni Maalumu baada ya kuhitimisha zoezi la uchangiaji.
Mgeni Maalumu Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Edward Ngoyai Lowassa akimkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye kuchangia katika Uzinduzi huo.
Mama wa pili na wa tatu kulia ni wawakilishi kutoka Kwaya Kuu ya Segerea.