Date: 
06-04-2017
Reading: 
Hebrews 7:23-27 (NIV)

THURSDAY 6TH APRIL 2017 MORNING                                   

Hebrews 7:23-27 New International Version (NIV)

23 Now there have been many of those priests, since death prevented them from continuing in office; 24 but because Jesus lives forever, he has a permanent priesthood. 25 Therefore he is able to save completely[a]those who come to God through him, because he always lives to intercede for them.

26 Such a high priest truly meets our need—one who is holy, blameless, pure, set apart from sinners, exalted above the heavens. 27 Unlike the other high priests, he does not need to offer sacrifices day after day, first for his own sins, and then for the sins of the people. He sacrificed for their sins once for all when he offered himself.

Footnotes:

  1. Hebrews 7:25 Or forever

The Jewish High Priests and Old Testament sacrifices were a shadow of what was to come. Jesus is both High Priest and a sacrifice. He sacrificed Himself once on the cross. His death was the perfect sacrifice to reconcile all people to God. When He died on the cross the curtain in the temple was torn from top to bottom showing that through Christ all can come freely into the presence of God.  Jesus truly reconciles sinful mankind and God who is Holy. 

ALHAMISI TAREHE 6 APRILI 2017 ASUBUHI                       

WAEBRANIA 7:23-27

23 Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu wazuiliwa na mauti wasikae; 
24 bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. 
25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
 26 Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu; 
27 ambaye hana haja kila siku, mfano wa wale makuhani wakuu wengine, kwanza kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kisha kwa ajili ya dhambi za hao watu; maana yeye alifanya hivi mara moja, alipojitoa nafsi yake. 
 

Makuhani wakuu na sadaka za wanyama katika Agano la Kale ni kivuli cha kifo cha Yesu Kristo msalabani. Yesu Kristo ni Kuhani Mkuu na sadaka pia. Yesu alijitoa msalabani mara mmoja kwa ajili ya dhambi za watu wote. Wakati alipokufa pazia katika Hekalu kuu lilipasuka toka juu hadi chini. Hii inaonyesha kwamba kupitia Yesu Kristo sote tunaweza kumkaribia Mungu. Yesu kweli ni mpatanishi kati binadamu wenye dhambi na Mungu mtakatifu.