Date: 
31-05-2019
Reading: 
Genesis 5:21-24 (Mwanzo 5:21-24)

FRIDAY 31ST MAY 2019 MORNING                                                       

GENESIS 5:21-24

21 When Enoch had lived 65 years, he became the father of Methuselah.22 After he became the father of Methuselah, Enoch walked faithfully with God 300 years and had other sons and daughters. 23 Altogether, Enoch lived a total of 365 years. 24 Enoch walked faithfully with God; then he was no more, because God took him away.     

God was pleased with Enoch. Enoch obeyed God in his life. His life was in harmony with God’s will and he walked in fellowship with God. Because of this God did not let Enoch taste death instead God took Enoch directly to heaven to be with Him.

Strive to live in harmony and fellowship with God day by day.  


IJUMAA TAREHE 31  MEI 2019 ASUBUHI                                            

MWANZO 5:21-24

21 Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. 
22 Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake. 
23 Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. 
24 Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa. 
 

Mungu alifurahia maisha ya Henoko. Henoko alimtii Mungu katika maisha yake. Henoko aliishi maisha yaliyompendeza Mungu na alikuwa na faragha na Mungu. Kwa sababu hii Mungu hakumruhusu Henoko kuona mauti. Bali Mungu alimchukua Henoko moja kwa moja Mbinguni kuishi naye.

Jitahidi kuishi kwa amani na Mungu kila siku.